WASICHANA WANG'ARA MATOKEO KIDATO CHA NNE...TAZAMA HAPA MATOKEO

 

Wasichana wameng'ara zaidi kwenye orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne 2021

Hayo yamebainishwa Januari 15, 2022 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde wakati akitoa taarifa ya matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne.

Matokeo hayo yanaonyesha wasichana wanane wameingia kwenye orodha ya wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliifanyika Novemba mwaka jana.

Kati ya hao, wasichana saba wanatoka shule ya St. Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya, msichana mwingine akitoka shule ya Bright Future Girls huku wavulana pekee walioingia kwenye kumi bora kitaifa wakitoka shule za Feza Boys ya Dar es Salaam na Ilboru ya Arusha.

Walioingia kwenye orodha hiyo ni pamoja na Consolata Lubuva, Buthoi Nkangaza, Wilihelmina Mujarifu, Glory Mbele na Mary Ngoso, wote kutoka shule ya St. Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya.

Bonyeza kila kiungio hapa chini kuona matokeo husika;

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments