Recent-Post

WATOTO WATATU WAFARIKI KWA KULA UYOGA NZEGA

 

 Katika hali ya kustaajabisha, watoto watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kudaiwa kula uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu katika eneo la Igombanilo, Nzega Mkoani wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema waliokula chakula hicho ni mama na watoto wake ambapo mpaka sasa mama na mtoto mmoja wanaendelea vizuri na wameruhusiwa kutoka Hospitali.

Kamanda Abwao amewataja waliofariki dunia ni Happiness Greyson, Annastazia Greyson na Maria Greyson.

Post a Comment

0 Comments