Watu 9 waaga dunia kwa kuzama baharini kisiwani Pemba, wengine hawajulikani waliko

             


  • Watu tisa wamefariki dunia na wengine kadhaa kuokolewa baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama Mkoa wa Kusini Pemba.

Ripoti zinasema boti hiyo iliyozama ilikuwa na wasafiri 30 waliokuwa wakitokea Chakechake kwenda kisiwa Panza kwa shughuli za mazishi.  

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud amesema ajali hiyo ilitokea jioni ya jana Jumanne baada ya chombo walichotumia kuwavusha kupata hitilafu na kuzama.

Amesema: "Mpaka sasa maiti tisa zimeopolewa, zipo hospitali ya Mkoani kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari ili baadaye taratibu za kukabidhi familia zao sitaendelea".

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba amesema hawajapata taarifa za chanzo cha ajali lakini taarifa za awali zinadai huenda ikawa ni idadi kubwa ya watu waliokuwa ndani ya boti hiyo kwa sababu hakuna uhakika walikuwa watu wangapi lakini ni kwamba walikuwa zaidi ya watu 30.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Mchomvu pia amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, mapaka jioni ya jana miili ya watu 9 ilikuwa imeopolewa na kwamba yote ni ya wanaume na watu wengine 6 wameokolewa. Amesema zoezi la uokoaji litaendelea leo asububi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments