Watu saba wameuliwa katika maandamano mapya Sudan

Jumuiya ya Madaktari wa Sudan imeripoti kuwa, polisi wa nchi hiyo wamewaua watu saba katika maandamano mapya dhidi ya utawala wa kijeshi nchini humo.

Madaktari wa Sudan wameeleza kuwa hadi sasa watu 71 wameuawa katika ghasia na mapigano kati ya askari usalama na wafanya maandamano huko Khartoum na katika miji mingine ya Sudan tangu kujiri mapinduzi nchini Oktoba 25 mwaka jana.  

Wafanya maandamano wanataka kuundwa serikali kamili ya kiraia na ya kidemokrasia huko Sudan. Sudan imetumbukia katika machafuko na mapigano kati ya askari jeshi na waandamanaji tangu baada ya wanajeshi kufanya mapinduzi tarehe 25 mwezi Oktoba mwaka jana na kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Abdallah Hamdok. Aidha jeshi lilimrejesha madarakani Hamdok baada ya kufikia muafaka wa kisiasa kati yake na Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al Burhan.

Abdallah Hamdok, Waziri Mkuu wa Sudan aliyepinduliwa na jeshi, na kurejeshwa uongozini baadaye 

 Umoja wa Mataifa pia umesema, unatiwa wasiwasi na kushtadi machafuko na umwagaji damu huko Sudan na kutahadharisha juu ya uwezekano wa kushuhudiwa maafa ya binadamu na njaa nchini humo. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments