Recent-Post

Waziri wa Fedha ateua wajumbe 11 Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)

 WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.Mwingulu Lameck Nchemba ameteua wajumbe 11 wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja uteuzi huo umeanza Desemba 19,2021.

Uteuzi huo unakuja kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua, Profesa Sylvia Shayo Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).

Katika uteuzi huo, Mheshimiwa Dkt.Mwingulu amewateua wafuatao kuwa wajumbe akiwemo Profesa Ganka D.Nyamsongoro, Bw. Issa Masoud Iddi,Bi.Aisha R.Kapande,Bw.Paul R.Bilabaye, Bw.Dyoya G.J. Dyoya, Bi.Rukia H.Abdulla, Bi.Rukia Adam,Bi.Witness Shilekirwa, Bw.Francis Mwakapalila, Bw.Fredrick B.Msumali na Bw.John Florian Ndetico.

Post a Comment

0 Comments