Recent-Post

YANGA 'MOTO'HAUZIMIKI YAICHAPA POLISI TANZANIA NA KUICHA SIMBA KWA POINTI 10

   

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeendelea na wimbi la ushindi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Tanzania Polisi mchezo uliopigwa katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid, jijini Arusha.

Shujaa wa Yanga ni winga mchachari aliyetokea benchi Dickson Ambundo aliwanyanyua washabiki wa Yanga dakika ya 64 akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha Pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 13 na kuwacha Simba kwa tofauti ya Pointi 10 ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na Pointi 25 kwa mechi 12 walizocheza.

Mchezo mwingine umepigwa katika dimba la Mkwakwani Tanga kwa wenyeji Coastal Union wamechezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC.

Mabao ya Obrey Chirwa dakika ya 37 huku mabao mawili yamefungwa na Reliants Lusajo yanamfanya kufikisha Mabao 7 na kumuacha Fiston Mayele akiwa na mabao sita na bao la kufutia machozi la Coastal limefungwa na Haji Ugando dakika ya 46.

Post a Comment

0 Comments