Bikizee mwenye umri wa miaka 102 kugombea urais NigeriaBikizee mmoja mwenye umri wa miaka 102 ametangaza nia ya kugombea urais wa Nigeria mwaka ujao wa 2023.
                             
Vyombo vya habari vya Nigeria viliripoti jana Aklhamisi kuwa, Nonye Josephine Ezeanyaeche ametangaza azma yake ya kugombea urais wakati alipotembelea Televisheni ya Taifa ya Nigeria (NTA).

Ezeanyaeche ambaye wengi wanamfahamu kwa lakabu yake ya ‘Mama Africa’ ni mzaliwa wa mji wa Aguata, jimboni Anambra na ni muasisi wa ‘Jumuiya ya Raia Wazee Nigeria.’

Akizungumza na waandishi habari, amesema yuko tayari kuwa rais wan chi iwapo vijana hawana azma ya kuongeza.

Nigeria haina kikomo cha umri kwa wanaotaka kugombea urais. Mwaka 2018 sheria ilipitishwa kuhusu  umri wa chini wa wanaotaka kugombea urais kuwa ni miaka 35.

Rais Buhari wa Nigeria
Rais Muhammadu Buhari hawezi kugombea tena urais wa Nigeria kwani anamaliza muhula wake wa pili.


Ezeanyaeche anaingia katika orodha ndefu ya waliotangaza azma ya kugombea urais wakiwa ni pamoja na mwenyekiit wa chama cha All Progressive Congress (APC) Ahmed Tinubu, gavana wa jimbo la Ebonyi, David Umahi na kiranja wa bunge la seneti Orji Uzor Kalu.

Mbali na uchaguzi huo wa rais mapema mwakani pia kutakuwa na uchaguzi wa magavana na wabunge katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments