CCM SINGIDA YAPIGA MARUFUKU KUFUKUZA WANACHAMA KIHOLELA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Juma Killimbah akivikwa Skafu na Skauti baada ya kuwasiri Ukumbi wa R.C. Mission kwa ajili ya sherehe hizo zilizofanyika juzi mkoani hapa.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia ukumbini kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita, Mbunge wa SingidaMjini Mussa Sima, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini Lusia Mwiru, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Killimbah, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu.

Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Singida Mjini,  Lusia Mwiru akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Sherehe zikiendelea.
Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima akizungumza wakati akitoa mada inayohusu Uzalendo.


Katibu wa CCM Mkoa wa Singida , Lucy Boniphace wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu na Katibu wa CCM, Lucy Boniphace wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu (kulia) akiwa kwenye maadhimisho hayo na makada wengine wa chama hicho. Katikati ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Idara ya Oganaizesheni Dafroza Lucas na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mandewa, Ramadhani Mtipa.

Mkuu wa Wilaya ya Manispaa ya Singida Mhandisi Pascas Muragili akitoa salamu za sherehe hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.

Sherehe zikiendelea. Kutoka kushoto ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Singida DC, Zainabu Abdallah, Katibu wa Mbunge wa Singida Kaskazini, Haruna Ntandu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Vijijini, Alexander Mboho na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ilongero, Rashid Ghambilu.
Sherehe zikiendelea.
Msanii Mussa Mashairi akitoa burudani.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo.
Sherehe zikiendelea. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mandewa, Baraka Hamisi.
Maadhimisho yakiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikipamba moto kwenye maadhimisho.
Furaha ikitawala kwenye maadhimisho hayo.
Makofi yakipigwa kwenye maadhimisho hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah amesema kiongozi yeyote wa chama hicho hana mamlaka ya kumfukuza mtu yeyote uanacha.

Killimbah ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo juzi wakati akihutubia katika maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM miaka 45 kwa mwaka 2022 Wilaya ya Singida Mjini.

"Mnapata wapi mamlaka ya kuwafukuza watu uanachama mwenye mamlaka ya kumfukuza mtu uanachama ni kikao pekee cha mkoa ambacho mwenyekiti wake ni mimi na sio vinginevyo ebu hayo matatizo yenu madogo madogo yamalizeni" alisema Killimbah.

Alisema kama kunakiongozi atakuwa amekosea wanaweza kumfukuza lakini sio mwanachama kwani ambaye anafukuzwa kwa taratibu zilizopo zikiwemo za kumuonya zaidi ya mara moja kwa kupitia kamati za maadili.

Akizungumzia mafanikio waliyopata katika kipindi cha miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho alisema kila wilaya imefanikiwa kujenga ofisi za kisasa za chama hicho huku akizitaja kuwa ni Mkalama, Iramba, Ikungi, Manyoni, Itigi, Singida Vijijini huku wilaya ya  Manispaa wakiendelea na mchakato wa ujenzi.

Killimbah alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi ya uongozi kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho utakaofanyika kuanzia Aprili 14 mwaka huu kwa kuanzia na vitongoji.

Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Singida Mjini,  Lusia Mwiru alisema changamoto kubwa iliyopo ni wanachama wengi kwa zaidi ya miaka miwili wamepigwa picha ili waweze kuingizwa kwenye mfumo wa kielekritoni baada ya kufanya taraibu zote lakini hadi leo hii hawajapata kadi zao jambo ambalo linawavunja nguvu hivyo aliomba suala hilo lishughulikiwe haraka.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 ya CCM nchi chini ya chama hicho imefanya mambo mengimakubwa ya maendeleo.

Alisema suala la kuongoza nchi sio la rahisi kama watu wengine wanavyo lifikiria na kuwa CCM ni Baba na Mama kwani kimetutoa mbali hivyo kila mtu anastahili kukipongeza.

Msita alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na watangulizi wake kwa kusimamia vizuri ilani ya chama kwa kusimamia nchi katika nyanja mbalimbali na kujenga imani kwa wananchi ya kuendelea kushika dola.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace alisema miongozo iliyoweka wakati wa maadhimisho hayo ni viongozi kuhamasisha wananchi kulipa kodi zikiwemo za majengo.

Katika maadhimisho hayo baadhi ya mambo yaliyofanyika ni kutembelea na kujionea eneo la ujenzi wa ukumbi na Ofisi ya CCM Wilaya, mada mbalimbali zilitolewa ikiwepo ya maadili ya viongozi, Mada ya Uzalendo iliyotolewa na Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima na maelezo mafupi ya maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM miaka 45 kimkoa. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments