CCM SINGIDA YAZINDUA RASMI KADI ZA KIELEKTRONIKI

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Killimbah akimkabidhi kadi ya Kielekrtroniki Amina Msaghaa wa Shina  Namba Moja  Sokoni Kata ya Ipembe wakati wa  uzinduzi wa  zoezi la ugawaji  wa kadi za Kielektroniki za chama hicho uliofanyika leo mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akizungumza wakati akizindua zoezi hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniphace akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Killimbah na Kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akichangia jambo wakati wa uzinduzi huo.
Uzibduzi ukifanyika.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah, akimkabidhi kadi hizo Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Shabani Hamisi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akimkabidhi kadi hizo Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba wakati wa zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akimkabidhi kadi hizo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ikungi, Bwanga Akida kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ikungi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akimkabidhi kadi hizo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akimkabidhi kadi  Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo akionesha kadi yake baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya Wenyeviti wa CCM na Makatibu wa wilaya wakiwa kwenye hafla ya kupokea kadi hizo.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah ameongoza zoezi la uzinduzi wa kadi za Kielektroniki za chama hicho mkoani hapa. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi hizo alisema CCM ni chama kikubwa ambacho hakiwezi kupitwa na chama chochote cha kisiasa hapa nchini na wakati wote kitaendelea kuwa mbele kutokana na mipango mizuri kiliyonayo.

Alisema uzinduzi unaofanyika leo ni muendelezo wa uzinduzi wa kitaifa uliofanyika wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya chama hicho uliofanyika mjini Musoma mkoani Mara ukiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.

"Tunachokifanya hivi sasa ni mabadiliko tunatoka kwenye mfumo wa kizamani wa analogia na kuingia kwenye mfumo wa kisasa wa kielekritoniki ambao utakisaidia chama chetu kupata Takwimu sahihi za Wanachama wake Kwa ngazi zote" alisema Killimbah. 

Alisema chama hicho kinapotimiza miaka 45 tangu kuzaliwa kwake kimefanya mambo mengi ya kujivunia na sasa kimeingia kwenye mabadiliko haya makubwa ya kuwa na kadi za kielektoniki ambayo yanakwenda na kasi ya maendeleo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniphace alisema hadi sasa wanachama waliosajiliwa kielektroniki kwa mkoa mzima ni 69,437 na kuwa zoezi hilo linaendelea kwa wilaya zote.

“ Hadi sasa wanachama waliosajiliwa kwa mfumo wa Kielektroniki ni 69,437 Wilaya ya Iramba ikiongoza kuwa na wanachama 16,709 huku ikiwa na wanachama 54,982, ikifuatiwa na Singida Vijijini, 13,767 ikiwa na wanachama 47,071, Ikungi 11,329 ikiwa na wanachama 51,471, Manyoni, 10,592 ikiwa na wanachama 81,183, Singida Mjini 10,086 ikiwa na wanachama 33,843 na Mkalama 6,954 ikiwa na wanachama 56,140 huku jumla ya wanachama wote ikiwa ni 324,690.

Alitaja idadi ya kadi zilizopokelewa katika kila wilaya ni Iramba, 2663, Singida Vijijini 2638, Ikungi 361, Manyoni 2572, Singida Mjini 1831 na Mkalama 391 jumla zikiwa ni 10,456. 

Aidha Boniphace aliagiza zoezi hilo la kusajili kieletroniki kasi yake iongezeke ili kila mwanachama ambaye hajapata kadi hiyo awe amepata kabla ya uchaguzi wa ndani ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments