CCM Utalingolo Watekeleza Dhima Ya Siasa Na Uchumi Kwa Vitendo

Katika kutekeleza dhima ya siasa na uchumi,Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Utalingolo kwa kushirikiana na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye ni diwani wa kata hiyo Erasto Mpete wamefanikiwa kupanda ekari moja ya miche ya matunda ya Parachichi.


Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji wa miche katika shamba la Chama lililopo katika kata hiyo amesema huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama chao cha Mapinduzi.

“Tumepanda miche katika shamba lenye wastani wa ekari moja ambayo imetosheleza miche 90,kimsingi huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba Chama lazima kiendane na uchumi,lazima kiwe na fedha”alisema Erasto Mpete

Aidha amesema utekelezaji huo ni agizo la kamati ya maendeleo ya kata ya Utalingolo (KAMAKA) kwa kila kaya kuwa na anagalau na miche 40 ya Parachichi huku taasisi ndani ya kata hiyo kuwa na angalau ekari moja ya matunda hayo lengo ikiwa ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,kaya na kata kwa ujumla.

“Utekelezaji huu pia ni agizo la kamaka,iliagiza kwamba kila kaya wawe angalau na nusu eka kwa maana ya miche 40 ya Parachichi lakini taasisi zozote zile angalau kuanzia ekari moja kwenda juu,rai yangu ni kuendelea kuhamasisha wananchi na taasisi zote ziweze kuiga mfano huu”alisema Mpete

Kwa upande wake Benigius Myonga (Suplius) ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Utalingolo,amewashukuru wanachama na diwani wa kata hiyo kwa ushirikiano mkubwa wanaouonyesha kwa kuwa awali hawakuweza kuwa pamoja.

“Awali kata yetu ilikuwa upinzani,awali hatukuwa pamoja na hatukuweza kuwa na vikao vya pamoja kwasababu kata yetu ilikuwa upinzani,na toka alivoingia Erasto Mpete ametuunganisha wote kwa pamoja na kufanikishia mawazo ikiwemo ya miradi”alisema Benigius Myonga

Nao baadhi ya wanachama wa Chama hicho akiwemo Aida Mbembati na Clavery Mlengule wametoa wito kwa wananchi wengine kuendelea na kilimo cha matunda hayo yenye soko kwa sasa ili kujikwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine Chama hicho chini ya mwenyekiti wake Benigius Myonga kimetoa shukrani za dhati kwa mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deodatus Mwanyika kwa kuwasaidia ghalama za miche hiyo,huku pia akishukuru kampuni ya Mtewele Genaral Traders kwa kufanikisha upatikanaji wa mbolea.


              Na Amiri Kilagalila,Njombe

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments