Chui aua mtoto, ajeruhi wanane

Mtoto Maganga Myeti (11) amefariki dunia baada ya kushambuliwa na chui katika Kijiji Cha Kakulingu wilayani Nzega huku watu wengine wanane wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea baada ya chui kutoroka katika Hifadhi ya Ipala

Ameeleza kuwa watu hao wanane waliojeruhiwa ni kutoka katika katika vijiji zaidi ya vitatu vinavyopakana na hifadhi hiyo.

"Chui huyo alivamia makazi ya watu saa mbili usiku baada ya kutoroka katika hifadhi," amesema.

Mnyama huyo alikuwa akikimbia ovyo kutoka kijiji kimoja hadi kingine na kujeruhi watu hao kwa nyakati tofauti.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Nzega Vijijini, Henerico Kanoga amesema tukio hilo limeathiri vijiji katika kata mbili za Milambo Itobo na Magengati.

Amesema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Mission ya Ndalla.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments