Huyu ndiye Rais wa Russia Vladmir Putin

 

Vita vya Vladmir Putin dhidi ya Ukraine vilianza kiongozi huyo alipokwenda kwenye televisheni ya Taifa na kutangaza “operesheni maalumu ya kijeshi”.

Upeo wake haukuwa wazi, lakini ushahidi wote uliashiria shambulio kubwa linakwenda kutokea. Putin alisema lengo ni kuondoa shughuli za kijeshi na “uchafu” katika nchi hiyo, akidai kuwa Ukraine ni tishio kubwa kwa Russia.

Ndani ya dakika chache baada ya tangazo hilo, milipuko ya makombora mazito ilisikika karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Kyiv, ambao ni mji mkuu wa Ukraine, na katika miji mingine mingi ya nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema inalenga tu maeneo ya kijeshi. Wanajeshi wa Russia waliripotiwa kutua miji mikubwa ya Ukraine ya Mariupol na Odessa, bandari mbili muhimu kwenye pwani ya Bahari Nyeusi ya Ukraine, ingawa ripoti hizi hazikuthibitishwa mara moja.

Pia, Putin alionekana kutishia matumizi ya nyuklia kwenye mzozo huo huku akizionya nchi za Magharibi, ambazo zimetuma wanajeshi kuimarisha ulinzi upande wa mashariki unaolindwa na Jumuia ya Kujihami (Nato) na kutishia vikwazo “vikubwa” vya kiuchumi, kuzionya nchi hizo kutoingilia vita hivyo.

Katika tangazo lake Putin alisema: “Nina maneno machache kwa wale wanaoweza kuhisi kushawishika kuingilia mambo yanayoendelea, yeyote anayejaribu kutuzuia, achilia mbali kutoa vitisho kwa nchi yetu na watu wake, lazima ajue kwamba jibu la Russia litakuwa la haraka na kusababisha matokeo ambayo hayajawahi kuonekana katika historia.”

Putin ni nani?

Rais wa Russia, Vladimir Putin alizaliwa mwaka wa 1952 huko St. Petersburg (wakati huo ikiitwa Leningrad). Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Leningrad, Putin alianza taaluma yake katika shirika la kijasusi la Russia (KGB) kama afisa wa ujasusi mwaka 1975.

Putin alipanda vyeo haraka katika Serikali ya Russia baada ya kujiunga na utawala wa Rais Boris Yeltsin mwaka 1998, na kuwa waziri mkuu mwaka 1999 kabla ya kuwa rais.

Putin aliteuliwa tena kuwa waziri mkuu wa Urusi mwaka 2008, na mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Rais wa Urusi.

Kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991, alistaafu kutoka KGB akiwa na cheo cha kanali, na akarudi Leningrad kama mfuasi wa Anatoly Sobchak (1937-2000), mwanasiasa huria. Katika uchaguzi wa mwisho kama Meya wa Leningrad (1991), Putin alikua mkuu wake wa kitengo cha uhusiano wa mambo ya nje na Naibu Meya wa kwanza (1994).

Baada ya kushindwa kwa Sobchak mwaka 1996, Putin alijiuzulu wadhifa wake na kuhamia Moscow. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Usimamizi katika utawala wa Rais wa Boris Yeltsin, akisimamia uhusiano wa Kremlin na Serikali za Mkoa.

Muda mfupi baadaye, aliteuliwa kuwa mkuu wa Usalama wa Shirikisho, ambalo awali lilikuwa ni tawi la iliyokuwa KGB, na Mkuu wa Baraza la Usalama la Yeltsin.

Agosti 1999 Yeltsin alimfukuza Waziri Mkuu, Sergey Stapashin pamoja na Baraza lake la Mawaziri, na kumpandisha cheo Putin kuchukua nafasi yake.

Desemba 1999 Yeltsin alijiuzulu urais, na kumteua Putin kukaimu nafasi yake hadi uchaguzi rasmi ulipofanyika mapema mwaka 2000. Alichaguliwa tena mwaka wa 2004. Aprili 2005 alifanya ziara ya kihistoria nchini Israeli kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Ariel Sharon, na hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi yeyote wa Kremlin.

Kwa sababu ya ukomo wa muda, Putin alilazimishwa kuacha urais mwaka 2008. Lakini alirudi kuhudumu kama waziri mkuu wa Dmitry Medvedevhadi 2012 alipochaguliwa tena kuwa Rais wa Urusi.

 Putin alitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi wa nchi

Rais wa Russia, Vladimir Putin amelitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi uliopo madarakani wa Rais Volodymyr Zelensky huku akiutuhumu kuwa wa kigaidi na genge la watumiaji wa dawa za kulevya. Soma zaidi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments