Recent-Post

Mamia wajitokeza mapokezi ya Dk Tulia Mbeya

 Mamia ya wakazi wa Jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi  katika Kata ya Nsalaga Jijini Mbeya kumpokea Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson huku Machifu  wakitoa neno la baraka na kumlinda.

Dk Tulia ambaye amewasilia Mkoani Mbeya Leo Jumamosi ,Februali 26, majira ya saa 9.45 alasiri.

Mara baada ya kuwasili  alipokewa  na Machifu wakiongozwa kiongozi wa machifu  Mkoa wa Mbeya ,Rocket Mwanshinga  viongozi wa  Serikali  na Chama akiwepo msanii wa kizazi kipya  kutoka Rebo ya Wasafi, Raimond  Mwakyusa (Rayvann).

Akizungumza mara baada ya kumpokea Spika Chifu Mwanshinga amesema kuwa Dk Tulia amerudi nyumbani na wako naye hawatamuacha kwani ni mtoto wao wamemkuza na kukemea mabaya yatakayothubutu kujitokeza.

''Tulia wewe ni mwanetu umekuja nyumbani tutakulinda  na tunakemea mabaya yote  mabaya juu yako ''amesema.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya, Aran Mwaigaga amesema kuwa Tulia ni Lulu  na dhahabu ya Mkoa wa Mbeya na mhimili wa Bunge na mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM ni wakati  wanachama waweke tofauti zao pembeni na kuweka  Maendeleo  ya Mkoa mbele.

'Nasema hivyo namaanisha kwani  Mkoa wa Mbeya Tangu nchi ipate Uhuru ni historia ya  kipekee kuwa na Mbunge na Spika Mwanamke sasa ni wakati wa kutumia ili Jiji liwe la kisasa na kijani''amesema.

Amesema kuwa ni wakati sasa chama kimefika hatua kiliyokuwa kikistahili kwa kuleta tija ya kukijenga kwa kuwa wamoja na kuunga mkono juhudi za Spika Dk Tulia Ackson  kwani wakati wa Maendeleo umefika.

Mkazi wa Uyole, Jane Samson amesema kuwa mapokezi ya Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ni kufuru kwani wameacha shughuli za kiuchumi na  kuungana na wanambeya  katika mapokezi.

 

Post a Comment

0 Comments