Recent-Post

Mbunge alia na bei za ATCL

Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu ameitaka Serikali kutafuta suluhisho la bei kubwa ya usafiri katika ndege za Shirika la Ndege Nchini (ATCL) ambapo amezifananisha gharama hizo na gharama za kwenda Dubai.

Mtaturu ameyasema hayo jana Jumanne Februari 15, 2022 wakati akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Amesema Shirika la ATCL limekuwa likifanya vizuri baada ya Serikali kulinunua ndege lakini limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Amesema bei ya tiketi ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma inafikia Sh400,000 hadi Sh700000, gharama ambayo ukiangalia ni kama abiria anakwenda Dubai.

Tumekuwa na changamoto kubwa kwa maana ya bei za tiketi. Ukiangalia tiketi ya kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma ni Sh400,000 hadi Sh700,000 ukiangalia wengine ni kama umeenda Dubai kumbe uko Tanzania hapa kumekuwa na changamoto lakini hakuna majibu,”amesema.

Mtaturu ameiomba Serikali kuangalia changamoto hiyo ya bei ya usafiri wa ndege.

Aidha, kumekuwa na malalamiko makubwa katika masuala ya mabando na kwamba mara nyingi wamewaeleza Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) waweze kuwasimamia watoa huduma kuhusu changamoto hiyo lakini haijafanyiwa kazi.

Leo unaweka bado la wiki moja ikiisha fedha zinaondoka wakati ulilipia mwenyewe. Wananchi wanalalamika, tunaiomba Serikali iwasaidie wananchi waweze kuwa na haki yao ya msingi katika wanapoweka bando,”amesema.

Amesema licha ya kuwasilisha changamoto hiyo TCRA limekuwa ni tatizo isiyokuwa na majibu hata wanapoulizwa watu wahuduma kwa wateja wamekuwa hawana majibu ya moja kwa moja.

Ameiomba Serikali kulifanyia kazi ili kuwapa haki wateja.

Post a Comment

0 Comments