Muhongo aiomba Serikali kufufua mradi wa Baba wa Taifa

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa, Sospeter Muhongo ameiomba Serikali kufufua mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Bugwema ulioanzishwa miaka ya 1970 na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Profesa Muhongo amedai kuwa mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji wa Bugwema una uwezo wa kulisha nchi nzima.

Akizungumza leo Jumapili Februari 6, 2022 kwenye uzinduzi wa mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari , Profesa Muhongo amemuambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mradi ukifufuliwa kutakuwa na uzalishaji wa mazao ya nafaka zikiwamo dengu, mahindi na mpunga..

"Huu ni mradi mkubwa sana ni skimu kubwa sana tunaomba Serikali iufufue kwani utakuwa na manufaa sio kwa Musoma pekee bali Tanzania nzima" amesema Profesa Muhongo

Amesema kuwa baada ya benki ya kilimo Tanzania kufanya utafiti ilibainika kuwa mradi huo utakuwa ni bora zaidi hivyo ni vema Serikali ikaufufua ili uanze kufanya kazi.

Kuhusu mradi wa maji Mugango- Kiabakari, Profesa Muhonho amesema kuwa kukamiliak kwa mradi huo utapeleka kwa mara ya kwanza wananchi wa jimbo lake kunufaika na mradi wa maji kutoka ziwa Victoria.

 Amesema kuwa hivi sasa ipo miradi mingi inayotekelezwa na Serikali kupitia Ruwasa katika vijiji 68 vya jimbo hilo huku akiongeza kuwa miradi mingi kati ya hiyo inategema maji kutoma ziwa Victoria.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa miradi hiyo bado kuna upungufu wa fedha na watumishi hivyo kuomba Serikali kufanyia kazi mapungufu hayo.

Akitoa maelezo kuhusu mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Anthony Sanga amesema kuwa mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 35 milioni za maji.

Amesema kuwa watu zaidi ya 195,000 katika vijiji 39 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo kutoka katika Wilaya za Musoma, Butiama na Bunda.

Ameongeza kuwa mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Unik kutoka nchini Lesotho ulianza mwezi Desemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu na kwamba hadi sasa umefikia asilimi 38 ya utekelezaji wake.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments