Recent-Post

Profesa Kitila: Mfumo wa elimu ufumuliwe, umepitwa na wakati

Mbunge wa Ubungo (CCM), Profesa Kitila Mkumbo amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume maalumu ya kuupitia mfumo wa elimu nchini, kwa kuwa mfumo wa sasa umepitwa na wakati.

Akizungumza wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na Mwananchi jijini Dodoma, Profesa Mkumbo amesema mfumo uliopo hauwafundishi wahitimu ujuzi wala stadi zozote za kujitegemea kimaisha, badala yake umelenga kumwezesha mwanafunzi kutoka ngazi moja kwenda ngazi inayofuata

Post a Comment

0 Comments