Rais Umaro Sissoco wa Guinea- Bissau jana usiku alitangaza kufeli na kugonga mwamba jaribio la mapinduzi nchini humo. |
Njama hiyo ya kutaka kuipindua serikali ya Guinea-Bissau imejiri wakati baraza la mawaziri wa nchi hiyo likifanya kikao cha dharura na Rais na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nuno Gomes Nabiam. Rais Umaro Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau ameeleza kuwa jaribio la mapinduzi lililokusudiwa kumuondoa madarakani lilifeli jana Jumanne na amewatolea wito wananchi kote nchini kuwa watulivu.
Akihutubiai taifa, Rais wa Guinea-Bissau ameeleza kuwa na hapa ninamnukuu" sikuwahi kufikiria kwamba kuna siku tutakumbwa na hali kama hii. Sikuwahi kudhania kwamba Waguinea-Bissau wanaweza kutekeleza kitendo kingine cha uibuaji machafuko," mwisho wa kunukuu
Rais Embalo wa Guinea-Bissau ameongeza kuwa, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vilifyatuliana risasi na wahusika wa jaribio la mapinduzi lililofeli kwa muda wa masaa matano kabla ya kusambaratisha njama hiyo.
Guinea Bissau baada ya jaribio la mapinduzi kufeli |
Rais wa Guinea-Bissau amesema ,anaamini kuwa wahalifu katika njama hiyo walikusudia kumuuwa yeye na mawaziri wengine wa serikali yake ambao walikuwa katika kikao chao cha kila wiki ikulu.
0 Comments