Rais Kenyatta atangaza rasmi kumuunga mkono Odinga katika uchaguzi wa rais Kenya

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza rasmi kumuunga mkono kinara wa chama cha upinzani cha ODM, Raila Odinga katika azma yake ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka huu.

Rais Kenyatta amesema hayo  katika mkutano wa wajumbe wa eneo la Mlima Kenya katika eneo la Sagana, yapata kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu Nairobi, ambayo ni ngome yake kuu ya kisiasa.

Ameiasa jamii ya Mlima Kenya impigie kura Odinga katika uchaguzi huo wa rais wa Agosti 9, akisisitiza kuwa kiongozi huyo mkuu wa upinzani atatanguliza mbele maslahi ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wakati huohuo, Rais Kenyatta ametumia jukwaa hilo 'kumpiga mabomu' naibu wake, William Ruto, ambaye pia anaendeleza kampeni za nchi nzima za kuwania urais.


Naibu Rais wa Kenyatta, William Ruto

Kenyatta ambaye anamaliza kipindi chake cha uongozi ndani ya miezi sita ijayo baada ya kuhudumu kwa mihula miwili, amesema haoni tatizo lolote kumuunga mkono Ruto katika chaguzi zingine zijazo, iwapo 'atabadilika.'

Baada ya tangazo hilo la leo, Kenyatta sasa anatazamiwa kujitosa rasmi katika kukurukakara za kisiasa kwa ajili ya kumpigia debe Odinga

                                                    

Post a Comment

0 Comments