RAIS SAMIA ATANGAZA NEEMA KWA WAWEKEZAJI KATIKA MAONESHO YA DUBAI EXPO 2020

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan wakati akielekea katika Banda la Maonesho la Tanzania lililopo Dubai leo tarehe 26 Februari, 2022. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, pamoja na wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika Siku ya Kitaifa ya Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yanayofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE leo tarehe 26 Februari, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania pamoja na la Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020 leo tarehe 26 Februari, 2022 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020 leo tarehe 26 Februari, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha kumbukumbu mara baada ya mazungumzo na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE na Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum leo tarehe 26 Februari, 2022. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania kwani kuna rasirimali nyingi na za kutosha hivyo muwekezaji atakaekuja kuwekeza Tanzania hatopata vikwazo ambavyo vitambana na kushindwa kuwekeza nchini.

Ametoa wito huo leo wakati akihutubia viongozi, pamoja na wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika Siku ya Kitaifa ya Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yanayofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE leo tarehe 26 Februari, 2022.

"Tanzania ni Nchi yenye amani na ina mazingira bora ya kuvutia wawekezaji hivyo nawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini". Amesema Rais Samia

Kupitia Maonesho hayo Tanzania imeweza kunufaika katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini, Utalii, Sekta ya mifuggo katika bidhaa za ngozi, fursa za uvuvi ambapo wavuvi wakubwa kuingia mkataba na serikali ya Zanzibar kwaajili ya kufanya shughuli ya uvuvi visiwani humo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments