Rais samia kufungua chuo cha taifa cha siasa

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia  kuzindua chuo cha Taifa cha Siasa ,Uongozi na maadili cha Mwalimu Nyeree ambacho kimejengewa  Kibaha Mkoani Pwani kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki vilivyopigania  ukombozi katika nchi za kusini mwa Afrika.

Chuo hicho  kimetajwa kujengwa kwa zaidi ya Sh100 bilioni, huku ikieelezwa kuwa hapo ndipo fikra za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo ili kupata  viongozi waliopikwa kizalendo.

Akitoa taarifa ya uzinduzi huo kwa waandishi wa habari leo Februari 19  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema Rais atazindua chuo hicho Februari 23 huku vyama shiriki vya ZANU -PF ya Zimbabwe, SWAPO ya Namibia , NBRA ya Angola , FLERIMO  ya Msumbiji na NPLL ya Angola zitashiriki kwenye uzinduzi huo.

"Chuo hiki kinamilikiwa na CCM kwa hiyo tumepata bahati Rais Samia Suluhu  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi anakuja kutuzindulia chuo chetu hivyo ni jambo la kushukuru  nawaomba wakazi wa Pwani kujitokeza kwa wingi siku hiyo"amesema

Kunenge ameongeza kuwa siku hiyo wageni mbalimbali wa ngazi ya mkoa, Taifa na nje ya nchi watakuwepo wakiwemo  makatibu wakuu wa vyama hivyo rafiki na watendaji wengine wa vyama hivyo.

Aidha Kunenge amesema kabla ya ujio wa Rais Samia siku hiyo, siku moja kabla kutakuwa na uzinduzi wa barabara yenye urefu wa kilomita mbili kwa kiwango cha lami utakaofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo.

Wakazi wa Kibaha kilipojengwa chuo hicho wamefurahia uwepo wake wakidai kimechangia wao kupata barabara ya kiwango cha lami ambayo imeondoa kero ya usafiri uliokuwepo awali kutokana na ubovu.

"Hii barabara leo ni lami, lakini mwanzo hatukua na lami yaani ilikua ni mbovu mno mbaya zaidi mvua ikinyesha ni tope hata pikipiki hazipiti hivyo tulikwama sana, chuo kimekuja na mambo mazuri ya lami"amesema  Jackson Yohana.

Hawa Seif ameongeza kuwa wajasiriamali wa mboga mboga wameweza kupata soko la biashara kwa sababu wateja wameongezeka tangu ujenzi wa chuo hicho ulipoanza na pia wimbi la vibaka limepungua kwa sababu  vijana wengi waliokua kijiwemi wamepata ajira eneo hilp ikiwemo ujenzi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments