RAIS SAMIA: WALIMU MAMBO MAZURI YANAKUJA

Serikali imeahidi neema kwa walimu huku ikiwataka waendelee kufanya kazi kwa moyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 7, 2022 wakati aliposimama wilayani Butiama kwaajili ya kusalimia wakazi wa wilaya hiyo.

"Walimu hoyeee, walimu mpo eehh sasa naomba niwaambie walimu mambo mazuri yanakuja endeleeni kuchapa kazi tumewajengea madarasa mazuri sasa kazi kwenu" amesema bila kufaganua zaidi.

Rais Samia amewataka wakazi wa wilaya ya Butiama kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiletea maendeleo huku akisema kuwa Serikali itaendela kushirikiana nai katika kuleta maendeleo.

"Nimewasikiliza wabunge wa mkoa wenu na ninachowambia ni kwamaba sisi tutaendelea kutoa fedha kwaajili ya maendeleo lakini wananchi nanyi lazima muendelee kufanya kazi, mkulima lima mfanyabiashara pia endelea " amesema

Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho kwaajili ya kuanz ujenzi wa soko la madini wilayani humo.

Dk Kiruswa amesema kuwa serikali inatambua mchango unaotokana na sekta ya madini hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa mazuri.

"Tunataka muwe na soko zuri kama wenzenu wa sehemu zingine kama vile Geita na hii itaboresha na kurahisisha shughuli zenu amesema" Dk Kiruswa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments