Recent-Post

Sakho, Aucho waleta vionjo vipya Bara


KOCHA wa Kagera Sugar, Francis Baraza, amewazungumzia mastaa wa Simba na Yanga, Pape Ousmane Sakho na Khalid Aucho namna walivyonogesha utamu wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kutokana na ubunifu wa kazi zaoBaraza alimtaja Sakho wa Simba kwamba licha ya kuchelewa kuonyesha madini ya mguu wake, mechi alizocheza vizuri ameona ubunifu na akili kubwa ya kazi, aliyonayo staa huyo, huku akimtarajia kufanya makubwa zaidi.

Kwa upande wa Aucho, alimuelezea ni mtaalamu wa kusambaza pasi, zinazoisaidia timu yake kuwa na umiliki wa mpira mbele ya wapinzani wao.

“Aina ya uchezaji wa Sakho na Aucho una vitu vinavyovutia macho ya wadau, kutazama kazi zao, mfano Sakho licha ya kutoanza mechi za kwanza za msimu bado anaonyesha Simba haikukosea kumsajili, akiendelea kucheza hivyo atakuwa habari nyingine,” alisema na kuongeza;

“Kuna wachezaji wengine kama Dickson Job wa Yanga, Reliants Lusajo (Namungo), Hassan Materema (Kagera Sugar), Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania) na Fiston Mayele (Yanga) na wenyewe wameonyesha kitu kikubwa msimu huu, ambacho kinafaa kuigwa na wengine, lengo ni kuifanya ligi kuwa tamu zaidi.”

Alisema ushindani wa ligi unavumbua vipaji vikubwa, akiwatolea mfano wazawa Job, Lusajo, Materema na Mayanga kwamba wataisaidia timu yao ya taifa kufanya vizuri.

“Napenda ushindani, ndani ya ushindani kuna burudani kali na wachezaji wanakuwa wanajitoa asilimia 100,” alisema Bara alizungumza Kagera akisema moto utawaka zaidi.

 

Post a Comment

0 Comments