Same kupanda miti 1,500,000

      

Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya maendeleo pamoja na taasisi za dini ina mpango wa kuotesha miche ya miti 1,500,000 kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo.

Miti huyo itaoteshwa kandokando ya barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam, ofisi ya Mkuu wa Wilaya, taasisi mbalimbali za Dini pamoja na shule zote za msingi na sekondari.

Miche hiyo imetolewa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya wilaya hiyo kiwamo,Wakala wa Huduma za misitu Tanzania wilayani Same (TFS) na taasisi ya Pangani Basin,

Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo amesema wamejipanga kuhakikisha katika msimu huu wa mvua wanabadilisha mazingira ndani ya wilaya hiyo na Same kuwa ya kijani.

Mpogolo amesema lengo la Serikali nikuhakikisha maeneo yote ya Hifadhi yanalindwa na kutunzwa huku akiwataka watendaji wa vijiji na Kata pamoja na wenyeviti wa vitongoji na vijiji ndani ya Wilaya hiyo wanasimamia sheria ya mazingira kwakushirikiana na kamati za mazingira kwenye Vijiji.

"Kweli huu ni msimu wa mvua nasisi kama Serikali kwakushirikiana na wananchi wetu tumejiwekea mikakati mbalimbali ya upandaji wa miti hii inajumuisha kila kaya kupanda miti mtano", amesema Mpogolo"

Mpogolo amesema watahakikisha maeneo yote yenye vyanzo vya maji hususani kwenye misitu ya asili yanaendelea kutunzwa na kuheshimiwa na kamwe hatavumilia uharibifu wa aina yeyote kwenye maeneo hayo.

Imeandikwa na Dickson Mnzava

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments