Serikali kuja na mpango mkakati kukomesha mauaji nchini

 Serikali imesema inaandaa mpango mkakati maalum wa kusaidia kukomesha mauaji ya watu mbalimbali yanayoendelea nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati kukiwa na matukio ya watu kuuliwa kikatili maeneo mbalimbali.

Haya yamesemwa leo  Alhamisi Februari 3, 2022 Bungeni na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa, Jeska Msambatavangu.

Akiuliza swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua mkakati wa Serikali kukomesha mauaji.

Akijibu swali hilo, Dk Gwajima amesema tayari wameanza kupeleka muongozo  kwa viongozi wa Vijiji kwa kutoa elimu na kuwekeana mkakati maalumu.

 Waziri amesema wataitumia Februari 6, ambayo ni siku ya kupinga ukeketaji ili kuzungumza na wananchi na kupeana mbinu za kumaliza mauaji hayo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments