Serikali yaondoa tozo ya petroli, dizeli, mafuta ya taa

Serikali imeondoa tozo ya Sh100 kwa kila lita ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Machi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Februari 28, 2022 na Wizara ya Nishati imesema kuwa sababu za kuondoa tozo hiyo ni kutokana na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine.

Pamoja na kwamba uamuzi huu utaipunguzia Serikali mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 30 kwa mwezi, Serikali imeona ni muhimu kuendelea kuwalinda wananchi wake dhidi ya athari za mabadiliko ya bei za mafuta ulimwenguni. Hii inatokana na ukweli kwamba endapo uamuzi huu usingechukuliwa na Serikali, bei za mafuta nchini kuanzia mwezi Machi na kuendelea zingekuwa za juu sans kutokana na sababu zilizoelezwa hapo juu” imesema taarifa hiyo

Taarifa hiyo imesema kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba ameidhinisha na kusaini marekebisho ya kanuni inayohusika na Tozo hiyo ili kutimiza uamuzi huu wa Serikali.

Uamuzi huu unaenda sambamba na maelekezo ya Mheshimiwa Sarnia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoyatoa baada ya kikao na Wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na suala hilo zilizokutana tarehe 5 Oktoba 2021 kujadiliana namna bora ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini na kupunguza tozo mbalimbali zenye thamani ya Shilingi bilioni 102 kwa watumiaji wa mafuta nchini

Bei mpya za mafuta zitakazotangazwa na Ewura na kuanza kutumika Machi2, 2022 zitazingatia marekebisho hayo ya kanuni yaliyofanywa na Waziri wa Nishati” imesema taarifa hiyo.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments