Recent-Post

Serikali yawataka Watanzani walioko Ukraine wahamie Poland, Romania


Wakati majeshi ya Urusi yakiendelea kuteka miji nchini Ukraine, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imewataka Watanzania zaidi ya 300 wanaoishi nchini humo kutafuta hifadhi katika nchi za Poland na Romania ambako kuna utulivu.  

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika wizara hiyo, Emmanuel Buhohela, leo Februari 27, 2022 imesema, Serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kwa Watanzania hao, hivyo nao watafute hifadhi.

Kutokana na hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Ukraine, Serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka ili Watanzania takribani 300 waliopo nchini humo kuondoka na kuingia katika nchi za Poland na Romania ambako kuna utulivu. Hatrua hii itatoa fursa kuwawezesha raia wetu kurejea nchini kwa usalama,” amesema Buhohela.

Aidha, Serikali imesema mpaka sasa hakuna Mtanzania yeyote aliyepata madhara kutokana na hali inayoendelea nchini Ukraine.
Ambapo wameomba wazazi wa wanafunzi, ndugu na jamaa wenye wapendwa wao nchini Ukraine, kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kuchukua hatua hizo.

Post a Comment

0 Comments