SIMBA SC YAENDELEA KUTAMBA KOMBE LA SHIRIKISHO, YAONDOKA NA ALAMA TATU DHIDI YA ASEC MIMOSAS

KLABU ya Simba Sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu kwenye kombe la Shirikisho hatua ya makundi mara baada ya kuichapa ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast kwa mabao 3-1.

Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza dakika ya 12 ya mchezo kupitia kwa kiungo wao Mshambuliaji raia wa Senegal Papa Sakho akifunga bao tamu na kuwanyanyua mashabiki ambao walikuwa wanashuhudia mechi hiyo kabambe.

Kipindi cha kwanza kiliisha huku Simba ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0, kipindi cha pili klabu ya ASEC Mimosas iliendelea kupambana kuweza kusawazisha bao kwenye mchezo huo kwa kufanya mashambulizi mengi na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Stephane Aziz Ki.

Licha ya ASEC Mimosas kusawazisha Simba Sc nao katika harakati za kushambulia kipa wa ASEC Mimosas alimchezea rafu Yusufu Mhilu na refa kuamuru ipigwe penati ambayo ilikwenda kupigwa na Shomari Kapombe na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Bao hilo lilidumu kwa dakika mbili tu za mchezo kabla ya Kiungo Mshambuliaji raia wa Malawi Peter Banda kugongelea msumari wa mwisho na kufanya matokeo kuwa 3-0 Simba ikiondoka na alama tatu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments