Sita wafukuzwa kazi Shinyanga

Watumishi sita waliokuwa wakifanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamefukuzwa kazi na Baraza la Madiwani kutokana na makosa ya kutoonekana kwenye maeneo yao ya kazi.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje ametangaza rasmi kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo Alhamisi Februari 24, 2022 katika ukumbi wa halmashauri hiyo katika kata ya Iselamagazi.

Amesema Baraza la Madiwani limewafukuza watumishi hao baada ya kupitia utetezi wao na   kujiridhisha, hivyo kuonekana baadhi yao kutoonekana muda mrefu katika maeneo yao ya kazi.

“Kutokana na sababu mbalimbali za kiutumishi baraza la Madiwani limewafukuza kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoka Idara ya Afya, watumishi wawili wamefukuzwa kazi na kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni wanne”amesema Mboje.

Licha ya watumishi hao sita kufukuzwa kazi, pia watumishi wengine wawili Baraza hilo limeagiza wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao, kwa muda wa miaka mitatu.

Mboje aliwataja watumishi hao waliofukuzwa kazi kuwa ni Daktari Fidelis Mushi wa Kituo cha afya Nindo na Andrew Israel Mwakisambwe ambaye ni Mteknolojia Maabara Kituo cha Afya Salawe.

Watumishi wengine ni wanne ni Utawala ambao ni Watendaji wa vijiji; Charles Dominick Mayunga (Bukene), Mercy Gasper Kyando (Kilimawe), Omary Hamis Omary (Igembya) na Robert Surika Mbuti (Mwabagehu).


Wakati huo huo mwenyekiti wa halmashauri hiyo amewaonya watumishi kuzingatia nidhamu katika ukusanyaji wa mapato, na utendaji wao wa kazi, ili kuwezesha kufikia malengo waliojiwekea, huku akiiomba serikali kusitisha kusomba mawe katika mgodi mpya wa Nyang'ombe iliyoko kata ya Mwakitolyo halmashauri ya Shinyanga.

"Kupitia baraza hili tunaiomba mamlaka inayohusika kudhibitisha mara moja kusomba mawe kuyapeleka katika halmashauri ya Nyang'wale mkoani Geita kutokana na kuwepo mgogoro wa mipaka hadi hapo utakapotatuliwa, ili kulinda mapato yao"amesema Mboje.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani Masalu Lusana wa Kata ya Mwakitolya na Sonya Jilala Kata ya Itwangi wameunga mkono hatua ya baraza hilo la kuwadhibiti wabadhirifu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments