Tetemeko la ardhi lazua taharuki Mpanda

Tetemeko la ardhi lililotokea  Ijumaa Februari 18, 2022 saa 2:12 usiku limezua taharuki kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda.

Tetemeko hilo ambalo limedumu takribani dakika tano limepiga katika maeneo ya Manispaa ya Mpanda ambapo bado hakuna taarifa za madhara zilizoripotiwa.

Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda, Silverius Komba (58) amedai kuwa tetemeko hilo ni kubwa tofauti na mengine ambayo amewahi kuyashuhudia.

"Nyumba imetikisika nikahisi tunakufa udongo umejaa ndani ilikuwa hatari sifahamu maeneo mengine hali ilikoje kutokana na uimara wa nyumba," amesema Komba akaongeza.

"Tulivyozoea imekuwa tofauti sana sijawahi shuhudia tetemeko kubwa kiasi hicho ikilinganishwa na lile lililotokea miaka miwili iliyopita,"

Akizungumza  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amethibitisha kutokea tetemeko hilo akisema bado hajapata ukubwa wa kipimo chake.

"Limepita maeneo yote tena ghafla hapa tunavyozungumza na wewe nipo maeneo ya mjini soko kuu mjini Mpanda kuangalia madhara yaliyojitokeza,"

"Lakini bado sijapokea taarifa za maafa yaliyotokea niombe wananchi waendelee kutoa taarifa vituo vya polisi walivyo karibu navyo,"

Amesema kwa kuwa limewashtua wengi yeye na kamati ya ulinzi na usalama wanaendelea kukusanya taarifa kila eneo ili kufahamu endapo kuna madhara yamejitokeza.

"Kweli nikubwa sana wengi wanadai haijawahi kutokea, nitakupa taarifa nikikamilisha uchunguzi wangu mwandishi," amesema Makame

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments