Recent-Post

TUME YA MADINI NDANI YA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI DAR ES SALAAM

    


Leo Februari 23, 2022 Tume ya Madini imeendelea kushiriki katika mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Watendaji wa Tume ya Madini walioshiriki ni pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Huduma za Tume, William Mtinya na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Dkt. Anorld Gesase.

Watendaji wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Henry Mditi, Mkurugenzi wa Manunuzi, Chenduta Makawa, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa.

Mkutano huo umeambatana na maonesho yenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini, biashara ya madini, mafanikio na majukumu ya Tume ya Madini.

Post a Comment

0 Comments