Shirika la Uuundaji Meli la Kenya (KSL) linalomilikiwa na Jeshi la Kenya limepokea oda sita kutoka Uganda na Tazania za kuziundia meli. |
Naibu Mkurugenzi wa KSL Kanali Peter Muthungu ameongeza kuwa tayari wamepokea oda zingine 11 kutoka mashirika ya ndani ya Kenya kwa ajili ya kuunda meli hizo.
Kanali Muthungu hakutaja gharama za kuunda meli moja huku akisema kuna mfumo wa kutathmini uundwaji meli kabla ya kubaini gharama.
Msemaji wa serikali ya Kenya Kanali Mstaafu Cyrus Ooguna amesema Shirika la KSL ndio la aina yake katika eneo na hivyo litaweza kutoa huduma kubwa nchini Kenya na katika nchi jirani.
Makao makuu ya Shirika la Uundaji Meli la Kenya yako katika Kituo cha Jeshi la Wanamaji cha Mtongwe, Mombasa na ni kituo cha kwanza cha aina yake. kusini mwa jangwa la Sahara na kilifunguliwa Disemba 2021 katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Tawi jingine la KSL liko katika bandari ya Kisumu katika Ziwa Viktoria na tayari kuna meli inayoundwa hapo yenye uwezo wa kubeba tani 1,800 ambayo itazinduliwa Aprili mwaka huu
0 Comments