Recent-Post

UN: Ukame Pembe ya Afrika umeua zaidi ya mifugo milioni 1.5


Ukosefu wa maji na maeneo ya malisho ni janga kwa mifugo na binadamu katika eneo la Pembe ya Afrika
                      

Hayo yamesema na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula FAO na kuongeza kuwa, mifugo milioni moja na laki tano imeteketea kutokana na ukame wa kupindukia na hivi sasa eneo hilo liko karibu mno kutumbukia kwenye janga jingine la kibinadamu. 

Reis Paulsen, mkurugenzi wa masuala ya dharura na uthabiti wa FAO aliyetembelea eneo hilo amesema kuwa, kuna wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuwasaidia watu wa ukanda huo na amesema, kwa uchache dola milioni 130 zinahitajika hadi mwezi Juni mwaka huu kuweza kuwaokoa watu wa Pembe ya Afrika na janga lisilotabirika ukubwa wake.


                           

Post a Comment

0 Comments