Wachimbaji Wadogo Wapewa Onyo

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe akizungumza na wachimbaji wadogo. Picha na Ernest Magashi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amewataka wachimbaji wa wadogo wadogo wa  madini ya dhahabu kuacha  udanganyifu wa kudanganya serikali katika matukio ya wizi wa kaboni na kutumia migodi kuwa kichaka cha kujificha.

Ametowa wito huo kwenye mgodi wa Rush ya Isanjabadugu kata ya Nyakafulu wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemery Senyamule ya kusikiliza kero za wachimbaji.

Mwaibambe amewaomba wachimbaji kuwa waminifu na kuaminiana ili kuepuka kuwekwa mikononi mwa vyomba vya dola kwa kuiba kaboni na kutorosha madini.

Alisema wimbi la wizi wa kaboni ambalo lilikuwa limepoa limerudi kwa kasi kwa kuzungukana wamiliki,ambapo Jeshi la Polisi lilibaini kwamba kaboni haiwezi kuibiwa na mtu ambae hajui matumizi yake.

Mwaibambe amesema “Tumekamata watu Kahama katika matukio mawili ya wizi wa kaboni yaliyo fanyika wilaya ya Mbogwe na tunaendelea kusaka mtandao huo”

Senyamule aliwaomba wachimbaji kuacha kujihusisha na mambo ya uhalifu badala yake wafichue waharifu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments