Wafanyakazi wa kutoa misaada na maafisa usalama watekwa nyara kaskazini mwa Cameroon

Wafanyakazi watatu wa kimataifa wa kutoa misaada ya matibabu wanaofanya kazi chini ya mwavuli wa Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) na maafisa wawili wa usalama wametekwa nyara usiku wa kuamkia leo katika jimbo la kaskazini mwa Cameroon.

Hayo yamethibitishwa na maafisa wa usalama wa eneo hilo ambao waseme kuwa, wafanyakazi hao wa misaada ya matibabu ni raia wa Ivory Coast, Chad na Senegal. Wametekwa nyara na watu wenye silaha wakiwa pamoja na walinzi wao wawili katika eneo la Fotokol, kaskazini mwa Cameroon.

Haikuweza kujulikana haraka ni nani hasa waliowateka nyara watu hao. Hata hivyo genge la kigaidi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara katika eneo hilo.

Maafisa wa serikali ya Cameroon wameanzisha operesheni za kuwatafuta na kimsingi jeshi la nchi hiyo ndilo lililopewa jukumu la kuwasaka na kuwakomboa watu wote hao watano.

Genge la Boko Haram limezidisha mashambulio yake dhidi ya raia katika eneo hilo tangu mwanzini mwa mwezi uliopita wa Januari. Hayo ni kwa mujibu wa maafisa usalama wa Cameroon.


Jumatano usiku wanamgambo wa Boko Haram waliua watu wasiopungua watatu katika eneo la jamii ya Ziler, kaskazini mwa Cameroon.


Magaidi wa Boko Haram wanaendesha vitendo vya kigaidi katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria. Lakini tangu mwaka 2015 walipanua wigo wa mashambulio yao na kuingia katika nchi jirani na Nigeria za Niger, Chad na Cameroon na wamekuwa wakisababisha maafa makubwa kwa wananchi wa kawaida wa hasa vijiji vya mbali ambako ni vigumu kufikiwa na wanajeshi wa serikali.



 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments