Watano wafa bajaji ikigongana na lori Mafinga

Watu watano wamefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki ya magurudumu matatu maarufu bajaji kugongana na lori katika eneo la Wambi Halmashauri ya mji Mafinga mkoani Iringa.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatano Februari 2, 2022 baada ya bajaji iliyokuwa na watu watano kugongana uso kwa uso na lori la kubebea magogo

Kwa mujibu wa mashuhuda, bajaji hiyo ilikuwa na watu watano akiwamo dereva ambapo wote walifariki dunia katika ajali hiyo.

Wamesema watu watatu ambao walikuwa kwenye lori akiwamo dereva wako salama.

Mwenyekiti wa madereva wa bajaji Mafinga mjini, Harouni Manga amedai kuwa ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva lori la magogo ambaye alikuwa anataka kupita gari la mbele yake hali ambayo imepelekea kuparamia bajaji hiyo na kusababisha vifo vya watu hao.

“Dereva wa lori alikuwa mzembe lakini kwa mujibu wa taarifa baada ya kufuatiliwa na Jeshi la Polisi walibaini kuwa dereva huyo alikuwa wamekunywa pombe hii ndio changamoto ya madereva wanaoendesha wakiwa wamelewa” amesema Manga

Manga amesema kuwa mili ya watu hao ilipelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Mafinga.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospital ya Mafinga, Dk Victor Msafiri amethibitisha kupokea kwa miili ya watu hao watano.

"Jana saa nne usiku nilipokea maiili ya watu watano wanaume wakiwa watatu na wanawake wawili” amesema Dk Msafiri

Dk Msafiri amesema hadi sasa miili yote imetambuliwa na ndugu zao kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kuwahifadhi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule ambaye amefika katika hospital ya Mafinga amewapa pole wafiwa na kutoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments