WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KWENYE SEKTA YA MADINI

      


Watanzania wametakiwa kuungana na wawekezaji kutoka nje ya nchi kwenye utoaji wa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini nchini ili waweze kunufaika huku Serikali ikipata mapato yake.

Wito huo umetolewa leo na Kamishna wa Tume ya Madini, Jenet Reuben Lekashingo kwenye mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

"Nia ya Serikali ni kuhakikisha watanzania wananufaika kwenye Sekta ya Madini, hivyo watanzania wanaweza kuingia makubaliano na wawekezaji kutoka nje ya nchi chini ya usimamizi wa Tume ya Madini na kuendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni za madini,"amesema Lekashingo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments