Zuhura Yunus ateuliwa Mkurugenzi mpya Mawasiliano Ikulu

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji laUingereza(BBC), Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano ya Rais -Ikulu.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Jumanne Februari Mosi 2022 imesema kuwa Zuhura anachukua nafasi ya Jaffar Haniuambaye atapangiwa majukumu mengine.

Taarifa hiyo imesema “Uteuzi huo umeanza Januari 30, 2022”

Hivi karibuni, Zuhura ambaye amepata umaarufu kupitia kipindi cha Dira ya Dunia cha BBC alitangaza mpango wake wa kuachana na shirika hilo na kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.

Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC zilikuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC mwaka wa 2008

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments