Recent-Post

Afariki akijaribu kumuokoa mchumba wake

Mtoto wa bilionea Juan Carlos Escotet Rodriguez mwenye umri wa miaka 31 amepoteza maisha wakati akijaribu kumuokoa mchumba wake wakati wa mashindano ya uvuvi mwishoni mwa wiki katika jimbo la Florida.

Kwa mujibu wa Magazine Espanol, mtoto huyo wa bilionea anayeitwa Juan Carlos Escotet Alviarez, ambaye ni mkurugenzi wa Banesco, alikuwa amepanga kumuoa mchumba wake, Andrea Montero mwezi Novemba.

Jarida la Miami Herald limeripoti kuwa mtoto huyo alifariki wakati akijaribu kumuokoa Montero aliyekuwa ameanguka kutoka kwenye boti yao ya urefu wa futi 60 wakati wawili hao wakishiriki shindano ya kuvua samaki lililoandaliwa na klabu ya Ocean Reef.

Herald limeandika kuwa baada ya kuingia majini, kijana huyo alipigwa na upanga wa boti hiyo na akafariki kutokana na majeraha aliyopata.

Gazeti hilo linamkariri mwandishi wa habari, Angela Oraa wa Venezuela akisema Montero aliweza kutoka majini bila ya matatizo.

Rodriguez ana utajiri unaokisiwa kuwa wa thamani ya dola bilioni 3.5 za Kimarekani na ni muasisi wa kundi la mabenki la Banesco ambalo limesambaza shughuli zake nchini Panama, Jamhuri ya Dominic, Puerto Rico, Colombia na Marekani.

Post a Comment

0 Comments