Ajali yaua saba Simiyu

Watu saba wamefariki dunia na wangine wanane wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha Lori ya saa moja na nusu jioni kugonga pikipiki ya matairi matatu (Bajaji) jana Jumapili March 27, 2022 katika eneo la mtaa wa Kidulya nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi Digital Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Simiyu, Faustine Mtitu amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa lori uliosababisha kugonga bajaji.

"Baada ya lori hilo kuigonga bajaji inayokisiwa kuwa ilikuwa imebeba abiria sita na lori likiwa na watu takribani 12, bajaji iliwaka moto na lori kupinduka," amesema Mtitu.

 By Samirah Yusuph Yusuph:Bariadi.

Post a Comment

0 Comments