Chad yamkabidhi kwa mahakama ya ICC kiongozi wa kundi la waasi wa Anti-Balaka

Serikali ya Chad imemkabidhi kiongozi wa kundi la waasi la Anti-Balaka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita na dhidi ya binadamu. Hayo yamethibitishwa na mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague Uholanzi.

Mahakama ya ICC imesema kuwa, Mokom anashukiwa kutenda na kuchochea jinai za kivita na dhidi ya binadamu zinazodaiwa huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye miaka 2013 na 2014.

Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mara ya kwanza ilitumbukia katika mgogoro mkubwa kuwahi kuiathiri nchi hiyo tangu ipate uhuru, baada ya kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Francois Bozize kupinduliwa madarakani na waasi wa kundi la Seleka mwezi Machi mwaka 2013. Kupinduliwa Bozize kuliibua wimbi la machafuko na mapigano kati ya kundi la Anti-Balaka na lile la Seleka.

Francois Bozize 

Jamhuri ya Afrika ya Kati ni moja ya nchi zenye uchumi dhaifu duniani licha ya kuwa na utajiri mkubwa maliasili yakiwemo madini mbalimbali. Si hayo tu bali Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa na historia ya machafuko tangu ipate uhuru wake kutoka kwa mkoloni Ufaransa mwezi Agosti mwaka 1960.  

Kundi la Kikristo la Anti-Balaka limehusika na  hujuma mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kama mauaji ya umati dhidi ya Waislamu, kuchoma misikiti na kushambulia makazi ya raia.  

 

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments