Recent-Post

Dk Mwigulu aiomba USAID dola 1.3 bilioni za Azaki

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ameliomba Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kutoa dola bilioni 1.3 zilizokuwa zitolewe kwa Asasi za Kiraia zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Waziri ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter akieleza kikao alichofanya kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Kate Somvongsiri, akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Emmanuel Tutuba.

“Nimeiomba @USAID kuelekeza msaada wa Dola 1.3 bilioni sawa na zaidi ya Sh3 trilioni inazotaka kuipatia Tanzania kupitia Asasi za Kiraia, zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita. Tutazisimamia vizuri,” ameandika Waziri Nchemba

Post a Comment

0 Comments