Dk Mwigulu asema benki ziliishiwa pumzi Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameifufua sekta ya fedha nchini baada ya kupitia kipindi kigumu japo haikuwahi kusemwa ambacho amesema benki nyingi ziliishiwa pumzi.

Mwigulu ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 5, 2022 katika uzinduzi wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.

“Nakupongeza sana kwa kazi kubwa unayofanya hapa nchini kwa upande wa sekta taasisi ya sekta za kifedha, umesaidia sana kuzifufua sekta za kifedha zikiwemo benki.

“Ilikuwa hayasemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Lakini malekezo yako na mabadiliko yako ya sera uliyochukua na hasa sera za matumizi zimewasaidia mabenki yetu kuweza kufufuka upya ulipoelekeza madeni ya ndani yalipwe wakati tunalipa madeni ya wazabuni, wakandarasa, watoa huduma.

“Miongoni mwa wale waliolipwa wapo ambao walikuwa wanadaiwa na mabenki yetu kwa hiyo kulipwa kwao na serikali kuliwafanya na wao wakalipe madeni yao kwenye mabenki,” amesema Dk Mwigulu.

Amsema baada ya Rais Samia alipoelekeza fedha nyingi ziende kwenye miradi ya maendeleo, maana yake fedha hizo zimeongezeka kwenye mzunguko na zimekutana na wale waliokuwa wanadaiwa kwenye benki na kuwezesha kulipa mikopo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments