Faru Rajabu afariki, TANAPA yathibitisha

 *Alikuwa na umri wa miaka 43

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limethibitisha kuwa, Faru Rajabu amefariki 
usiku wa kuamkia leo Machi 21,2022 akiwa na umri wa miaka 43.

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa faru maarufu aliyejulikana kama Faru John aliyefariki mapema mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 47.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelutete inaeleza kuwa Faru Rajabu alifariki katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni uzee.
“Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linasikitika kutangaza kifo cha Faru Rajabu mwenye umri wa miaka 43 kilichotokea usiku wa kuamkia leo kutokana na sababu ya uzee katika Hifadhi ya Taifa Serengeti,” imeeleza sehemu ya taarifa ya TANAPA.

Kwa mujibu wa TANAPA mwili wa faru huyo utahifadhiwa kwa mujibu wa kanuni za asili za uhifadhi.

Faru Rajabu ambaye alizaliwa kwenye eneo Ngorongoro mwaka 1979 na mwaka 1993 alihamia katika Hifadhi ya Serengeti ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.
CHANZO NA DIRAMAKINI

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments