Hapi: Kinana ni mtu mwenye uwezo mkubwa


  Mkuu wa Mkoa wa Mara,  Ally Hapi amesema kuwa Abdulrahman Kinana ambaye jina lake limependelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kuwataka kuachana na mambo ya nyuma.

Kauli yake hii inakuja kutokanana na swali aliloulizwa na wanahabari nje ya ya ukumbi wa Jakaya kikwete unakofanyika mkutano mkuu wa CCM jijini dodoma ambapo amesema kuwa mambo yaliyopita hayana msingi kwa sasa.

"Hakuna ubishi juu ya uwezo wa Mzee Kinana" ameeleza  Hapi

Hapi ameeleza kuwa Kinana ni mtu mwenye uwezo, maarifa na uzoefu mkubwa kwenye siasa na ni mwalimu kwa watu wengi kwenye chama hicho.

"Kama vijana ambao tunaendelea kujifunza kwenye siasa za chama mambo ya nyuma nadhani hayana msingi kwa sasa hivi" aliongeza

Mangula ang’atuka, Kinana kumrithi

Post a Comment

0 Comments