Katika kipindi cha mwaka mmoja Rais, Samia Suluhu Hassan ameidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 12.4 katika sekta ya afya wilaya ya ikungi katika miradi mipya ya Ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya na zahanati pamoja na mishahara ya watumishi sekta ya afya
Tumeidhinishiwa milioni 800 umaliziaji wa hospitali mpya ya wilaya ujenzi uko asilimia 80, tumeidhinishiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vinne vipya vya afya Iyumbu fedha za umaliziaji, iglanson, ntuntu, na irisya
Pamoja na kuidhinishwa fedha hizo pia tumepokea fedha Milioni 200 ajili ya ujenzi wa zahanati mpya katika vijijini vinne pamoja na fedha za dawa na vifaa tiba na mishahara ya watumishi katika sekta ya afya
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi ambayo yalikaguliwa na Wananchi wakati wa maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa madarakani. |
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Stamili Dendegu akizungumza kwenye hafla hiyo wakati akimkalibisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Mika Likapakapa. (hayupo pichani) |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akihutubia katika hafla hiyo. |
0 Comments