Kadhaa wauawa katika shambulio la waasi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Watu wasiopungua watano wameuawa baada ya genge moja la waasi kushambulia kambi ya jeshi huko mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hayo yalisemwa jana Alkhamisi na Jean Ulrich Semberkpanga, naibu kiranja wa eneo la Ouham-Pende na kuongeza kuwa, raia watatu wakiwemo wanawake wawili ni miongoni mwa watu waliouawa katika hujuma hiyo ya waasi.

Aidha wanajeshi wawili wa serikali  ya CAR wameuawa katika shambulio hilo lililotokea katika mji wa Nzakoungou, katika mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Chad na Cameroon.

Maafisa usalama katika eneo hilo wamesema genge la waasi la 3R (Return, Reclamation, Rehabilitation) ndilo lililofanya mauaji hayo. Mbali na watu watano kuuawa katika hujuma hiyo, wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Wakazi wa kijiji kilichoshambuliwa wanasema wanachama wa kundi la 3R linalodai kupigania maslahi ya jamii ya Fulani waliingia kijijini hapo na kuanza kufyatua risasi ovyo na kuua watu watano na kujeruhi wengine wengi.

Jamhuri ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa madini imekuwa katika mgogoro na mapigano ya kidini na kikabila tokea mwaka 2013.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments