KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MKAKATI WA KUKUZA KILIMO CHA MKONGE,WAPONGEZA GHARAMA NDOGO UKARABATI WA JENGO LA BODI YA MKONGE

    




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kikimo,Mifugo na Maji imeipongeza serikali kwa mikakati yake madhubuti ya kuinua zao la mkonge nchini na kuridhishwa na hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na serikali katika kuongeza uzalishaji wa Mkonge kufikia tani 120,000 ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji *Dr.Christine Ishengoma* wakati za ziara ya kamati kukagua ukarabati wa jengo la ofisi ya Bodi ya Mkonge na kutembelea wasindikaji na wakulima wa mkonge katika Wilaya za Muheza na Korogwe.

“Hili jengo limejengwa mwaka 1840,lakini ukarabati huu umelifanya liwe na taswira tofauti ya kuvutia.Ukarabati huu umetumia kiasi cha *Tsh 506m* katika hatua hizi mbili za awali gharama ambayo usingeitemea kutumika kutokana na hali ya uchakavu wa majengo haya.

Tunaiona mikakati mizuri ya serikali katika kuchochea uzalishaji wa zao la mkonge,tunapongeza jitihada hizi na sisi kama kamati ya bunge tutatoa ushirikiano kuhakikisha tunafikia malengo ya kukuza tasnia hii ya mkonge.

Serikali lazima ihakikishe inasimamia vyema zao hili kwa kutatua changamoto zinazowakabili wakulima ili wakulima wa zao hili wanufaike na kilimo chao”Alisema Dr. Ishengoma

Akijibu changamoto za wakulima,Naibu Waziri wa Kilimo *Mh Anthony Mavunde* amebainisha mikakati ya serikali katika kukuza zao la mkonge ikiwemo ununuzi wa korona mpya za kisasa ili zisaidie kusindika mkonge mwingi kwa wakati muafaka tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mkonge mwingi wa mkulima hukaukia shambani kwa kushindwa kuvunwa kwa wakati na hivyo kupelekea hasara kwa mkulima.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania *Ndg. Saddy Kambona* amesema kwamba mpango wa sasa wa Bodi ni kuhakikisha wanaongeza uzalishaji kuwa mkubwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya masoko mbalimbali ya nje ya nchi hali ambayo itasaidia kukuza pato la Taifa na kuinua uchumi wa wakulima.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments