Kesi za maambukizi ya corona zaongezeka Nigeria baada ya wanafunzi kurejea nchini wakitokea Ukraine

Nigeria imetangaza ongezeko la maambukizo ya Covid-19 siku moja baada ya kusajili idadi ndogo zaidi ya kila siku iliyorekodiwa tangu kuanza kwa janga hilo.

 Siku ya Jumatatu iliyopita Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria kilitangaza visa viwili pekee vilivyorekodiwa nchini humo vya maambukizi ya corona.

Siku ya Jumanne mamlaka ya afya ilirekodi maambukizo mapya 118 ya COVID-19.

Ongezeko hilo la waathirika wa virusi vya corona linahusishwa wka sehemu moja na kurejea nchini  Wanigeria 772 waliokimbia vita nchini Ukraine ambayo kwa sasa inapigana na Russia.

Wanigeria wasiopungua 60 waliorejea nchini kutoka Ukraine wamepatikana na virusi vya corona.

Tamwimu zinaonesha kuwa,Wanigeria 3,142 wameaga dunia kutokana na ugonwja wa COVID-19 wakati idadi ya walioambukizwa imeongezeka hadi 254,861.

Afrika Kusini inaongoza barani Afrika kwa kuwa na waathirika 3,688,423 wa corona. Zaidi ya raia 99,656 wa nchi hiyo wameaga dunia kutokana na virusi hivyo. Nchi nyingine zilizoathiriwa sana na virusi vya corona barani Afrika ni Morocco, Tunisia, Misri, Ethiopia, Libya na Kenya.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa, itakuwa kosa kubwa kudhani kuwa ugonjwa wa COVID-19 umekwisha.

Zaidi ya watu miloni 446 duniani kote wamembukizwa COVID-19 hadi sasa na kati yao zaidi ya milioni 6 wamepoteza maisha na wengine wengi afya zao za akili zinazorota.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments