KISHINDO CHA MWAKA MMOJA WA UWONGOZI WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMA SAMIA SULUHU HASSANI

Kwa Sensa Ya Mwaka 2012, Vijana Wa Singida Ni 822,382 Sawa Na 60% Ya  Wakazi Takribani 1,370,637.Hivyo Wanufaika Wa Kwanza Wa Miradi Yote Ya Maendeleo Ni Vijana, Rais wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Ameeongeza Mikopo Ya Elimu Ya Juu Toka Bilioni 464 Hadi Billioni 570 Sawa  Na Ongezeko La Bilioni 106 IkiwaNi Ongezeko La  Wanufaika 18,000;;; Leo migomo Ya Vyuo Na Vyuo Vikuu  Ni Hostoria Tena Tanzania.

Kauli Hiyo Imesemwa Na Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Ccm Mkoa Wa Singida(UVCCM) DR. Denis Nyiraha Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Katika Ukumbi Wa Chama Cha CCM Mkoa Wa Singida mnamo tarehe 2-03-2022.

 Dr. Nyiraha Ameeleza Ndani Ya Mwaka Mmoja Wa Rais Samia Katika Uongozi Wake Jumla Ya Vikundi 221 Vya Vijana Vimenufaika Na Mikopo Ya Asilimia 4% Ya Mapato Ya Halmashauri ,Hivyo Kufikia Lengo Kwa Asilimia 90% Mkoani Singida

Aidha Mwenyekiti Uvccm Mkoa Wa Singida Denis Nyiraha Amesema Kuwa Nchi Yetu Imebarikiwa Kwa Kuwa Na Rais Ambaye Ni Mama Mlezi ,, Mmama Mchapa Kazi Na Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania ,Tutegemee Mwendelezo Wa Malezi Bora ,Kishindo Na Uongozi Mathubuti ,Mpaka Sasa Rais Samia Amelipia Ndege 5 Ili Kuendelea Kuimarisha Shirika La Ndege ATCL Na Katika Ndege  Hizo Moja Ni Ya Mizingo (Cargo).

Na  Abdul Bandola  Singida

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments