KOCHA 'GUARDIOLA' AWAPA ZAWADI YA MAHINDI YA KUCHEMSHA WACHEZAJI WA LA MASIA FC

 


USHINDI una raha yake bwana asikwambie mtu! Mkoani Iringa wikiendi iliyopita ilipigwa mechi ya kibabe kati ya La Masia FC dhidi ya Mbuni FC mchezo uliomalizika kwa La Masia kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Mabao ya La Masia kwenye mchezo huo yaliwekwa kambani na Meckson Juma aliyefunga mawili dakika ya 10 na 25, Ally Kombo 50, Peter Mwakalinga dk 70 na 85 mabao ambayo yameifanya timu hiyo kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Baada ya mchezo kumalizika Kocha wa La Masia FC, Muhidin Muhidin ‘Guardiola’ aliwanunulia wachezaji wake mahindi ya kuchemsha kama sehemu ya kuwapongeza kwa dozi nzito waliyoitoa kwa Mbuni FC ambao walikula mkono mwanagu.

Post a Comment

0 Comments